1. Taarifa za Mteja
Mteja anatakiwa kutoa taarifa sahihi wakati wa kuweka order, ikiwemo jina, namba ya simu, anwani na taarifa nyingine zinazohitajika kwa delivery.
GAMORA ONLINE
Kwa kutumia GAMORA ONLINE, unakubaliana na vigezo na masharti haya. Tafadhali yasome kabla ya kuweka oda.
Ilisasishwa: Agosti 2026
Mteja anatakiwa kutoa taarifa sahihi wakati wa kuweka order, ikiwemo jina, namba ya simu, anwani na taarifa nyingine zinazohitajika kwa delivery.
Oda inayowekwa kupitia tovuti inaweza kukaguliwa kabla ya kuthibitishwa. GAMORA ONLINE inaweza kuwasiliana na mteja kuthibitisha order ikiwa taarifa zaidi zinahitajika.
Bei zinazoonyeshwa kwenye tovuti zinaweza kubadilika. Bei itakayoonyeshwa wakati wa kuthibitisha oda ndiyo itatumika, isipokuwa pale ambapo kuna hitilafu ya wazi ya mfumo au bei.
Njia za malipo zitakazoonekana wakati wa malipo ndizo zitakazotumika. Mteja anatakiwa kuhakikisha taarifa za malipo ni sahihi na salama.
Uwasilishaji unaweza kuhesabiwa kulingana na umbali na eneo la mteja. Muda wa delivery unaweza kutofautiana kulingana na eneo, msongamano wa magari, hali ya hewa na sababu nyingine za usafirishaji.
Tunajitahidi kuhakikisha taarifa za bidhaa, picha, bei na upatikanaji wa bidhaa ni sahihi. Hata hivyo, kunaweza kutokea tofauti ndogo kwenye picha au maelezo ya bidhaa.
Maombi ya cancellation au marejesho yatashughulikiwa kulingana na hali ya order na sera ya bidhaa husika. Mteja anatakiwa kuwasiliana na GAMORA ONLINE mapema iwezekanavyo.
Mteja hatakiwi kutumia tovuti kwa shughuli haramu, udanganyifu, kuharibu mfumo au kujaribu kupata taarifa ambazo hana ruhusa nazo.
GAMORA ONLINE inaweza kubadilisha masharti haya inapohitajika. Toleo jipya litachapishwa kwenye tovuti.
Kwa maswali kuhusu masharti haya, wasiliana nasi kupitia simu, WhatsApp au njia nyingine rasmi za mawasiliano zilizowekwa kwenye tovuti.
Kwa maswali kuhusu masharti haya, wasiliana nasi kupitia simu, WhatsApp au njia nyingine rasmi za mawasiliano zilizowekwa kwenye tovuti.